FAIDA YA PARACHICHI KWA WATOTO


Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Parachichi ni tunda lenye virutubisho vingi ambavyo ni muhimu sana kwa afya ya watoto. Watoto wanapokua wanahitaji vyakula vyenye nguvu na vitamini ili miili na akili zao zikue vizuri. Moja ya tunda linalofaa kwa ukuaji wao ni parachichi.

Parachichi lina mafuta mazuri yanayosaidia ukuaji wa ubongo. Watoto wanaokula parachichi mara kwa mara huwa na uwezo mzuri wa kukumbuka na kujifunza mambo mapya shuleni.

Zaidi ya hayo parachichi lina nyuzinyuzi zinazosaidia mmeng’enyo wa chakula. Hii inawazuia watoto kupata matatizo ya tumbo kama kuharisha au kufunga choo.



Parachichi pia husaidia kuongeza kinga ya mwili kwa watoto. Vitamini C na virutubisho vingine vilivyomo huimarisha mwili ili uweze kupambana na magonjwa kwa urahisi. Aidha parachichi ni rahisi kuliwa kwa kuwa ni laini hivyo hata mtoto mdogo anaweza kulila bila tabu.

Kwa jumla parachichi ni tunda lenye faida kubwa kwa watoto. Wazazi wanapaswa kuhakikisha watoto wao wanakula parachichi mara kwa mara ili wawe na afya bora akili nzuri na miili yenye nguvu. Hakika parachichi ni hazina ya afya kwa watoto.

 

 

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872

 

 

0/Post a Comment/Comments