Emakulata Msafiri,
Mwanakwetukids.
Katika kijiji kidogo cha aliishi msichana mdogo aitwaye Amina. Amina alizaliwa bila uwezo wa kuona, lakini moyo wake ulikuwa umejaa ndoto. Alipenda sauti za hadithi, alizozisikia kila jioni kutoka kwa babu yake aliyekuwa akimwambia simulizi za mashujaa, wanyama, na safari za ajabu. Kila mara alipomsikia babu akisema, “Soma kitabu hiki, utaelewa zaidi,” Amina alitamani kujua kusoma ni nini?,
Siku moja, walimu kutoka shirika la watoto wenye ulemavu wa kuona walifika shuleni. Walileta vitabu vya maandishi ya nukta nundu (Braille). Wanafunzi wengi walishangaa, lakini kwa Amina, ilikuwa kama mlango mpya umefunguliwa. Alipohisi nukta hizo ndogo kwa vidole vyake, moyo wake ulijawa na furaha. Alijua kwamba hatimaye, hata yeye anaweza kusoma kwa macho ya moyo.
Lakini changamoto zilikuwa nyingi. Shule yao haikuwa na vitabu vya kutosha vya Braille, na mwalimu mmoja pekee ndiye aliyekuwa amepata mafunzo ya kuwasaidia watoto wenye ulemavu wa kuona. Wakati wengine walikuwa na madarasa yenye mwanga na madawati mazuri, Amina na wenzake waliketi chini ya mti. Hata hivyo, hamu yao ya kusoma haikupungua.
Kila siku Amina alisoma ukurasa mmoja zaidi. Alijifunza kuhusu sayansi historia na hata mashairi. Aligundua kuwa ulemavu wa kuona haukumzuia kuwa na ndoto kubwa. Aliamini kwamba elimu ni haki ya kila mtoto iwe anaona au haoni anatembea au anakaa kwenye kiti cha magurudumu.
Miaka ilipita na Amina akawa mwalimu. Alifundisha watoto wengine wenye ulemavu wa kuona kusoma na kuandika kwa Braille. Mara nyingi aliwaambia:
“Ulimwengu unaweza kuwa giza kwa macho lakini elimu uangaza ndani ya moyo.”
Kupitia jitihada zake, serikali ilianza kujenga maktaba maalum zenye vitabu vya sauti na Braille. Watoto wengi zaidi walipata nafasi ya kusoma na kufuata ndoto zao.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872
Post a Comment