Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Hapo zamani kidogo, kulikuwa na familia iliyokuwa ikiishi Mbeya. Familia hiyo ilikuwa na baba anayeitwa Paulo, mama anayeitwa Anna na watoto wao wawili Neema na Tuma.
Neema alikuwa msichana mkubwa mwenye bidii na mtiifu. Lakini Tuma ambaye alikuwa mdogo wakealikuwa na tabia ya kupenda michezo zaidi kuliko kusaidia kazi za nyumbani.
Kila siku baba yao alikwenda shambani kulima na mama yao akibaki kupika na kufua nguo. Neema alikuwa akimsaidia mama yake lakini Tuma mara nyingi alikimbilia kucheza na marafiki zake karibu na mto.
Siku moja hali ya hewa ilibadilika. Upepo mkali ulianza kuvuma mawingu makubwa yakajaa angani. Baba yao alikuwa bado shambani Mama akawaambia watoto wake wasaidiane kufanya kazi haraka haraka.
Neema akakimbia kuchukua nyasi na kamba lakini Tuma akasema, “Ah mama upepo utapita tu si lazima nifanye kazi sasa.”
Wakati Tuma akicheka upepo ulianza kuongezeka. Ghafla sehemu ya paa likaanza kung’oka! Neema akamuita Tuma kwa sauti ya hofu, “Njoo tusaidiane haraka nyumba yetu inaweza kuharibika!”
Tuma alipomuona dada yake akihangaika alihisi aibu. Akaacha michezo na kukimbia kumsaidia. Kwa pamoja walishikilia paa kwa nguvu wakisaidiwa na mama yao. Walifanikiwa kulilinda paa hadi upepo ulipopungua.
0653903872
emakulatemsafiri@gmail.com

Post a Comment