BINTI MWEREVU NA KIJIJI CHA KIU

 Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Kulikuwa na kijiji kimoja kilichoitwa Kijiji cha Lwoga. Kijiji hiki kilikuwa na shida kubwa ya maji. Mto ulikauka, visima vilikauka na watu wakaanza kuhama kwenda mbali kutafuta maji.

Lakini kulikuwa na binti mdogo mwenye akili nyingi aliyeitwa Zawadi. Alikuwa na miaka kumi na mbili tu lakini moyo wake ulikuwa mkubwa kuliko umri wake. Siku moja akaenda kumwona mzee wa mila akamwambia nina ndoto kuwa maji yapo karibu tu lakini tumekuwa tukitafuta mbali.”

Mzee akacheka akasema “Binti maji yamekauka kila mahali si rahisi kuyapata tena.”

Lakini Zawadi hakukata tamaa. Alikusanya vijana wachache wa kijiji wakaenda kwenye sehemu ambayo aliona kwenye ndoto yake. Walipochimba kwa siku tatu tu wakapata chemchemi kubwa ya maji safi!

Wakazi wote wa kijiji walifurahi sana. Wakampongeza Zawadi na kumuita “Binti wa Maji”. Kuanzia siku hiyo watu walijifunza kwamba. “Ujasiri na imani vinaweza kuleta suluhisho hata pale ambapo watu wamekata tamaa.”

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments