BIDII HUSHINDA HALI NGUMU YA MAISHA

 

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Kijijini Iringa kulikuwa na msichana anayeitwa Asha. Alitoka kwenye familia maskini. Wazazi wake walikuwa wakulima na mara nyingi hawakuwa na pesa za kutosha hata za mahitaji ya msingi. Lakini licha ya hali hiyo Asha alipenda sana kusoma.

Kila siku baada ya kurudi shuleni alikaa kwenye kivuli cha mti akiwa na daftari moja tu ambalo lilikuwa limechakaa. Wakati watoto wengine walikuwa wakicheza au kupoteza muda Asha alikuwa akisoma na kuandika maneno aliyojifunza darasani.

Siku moja mwalimu wake alimuuliza.“Asha kwa nini unapenda kusoma sana?”

 “Nataka siku moja niwe mwalimu au daktari ili niwasaidie wazazi wangu na watoto wa kijijini wasiteseke kama sisi.”

Maneno yale yaliwagusa wengi na baadaye mwalimu na wanakijiji walichanga pesa kidogo kumpatia vitabu na madaftari vipya. Asha aliendelea kusoma kwa bidii na hatimaye alipomaliza shule ya msingi alipata nafasi ya kusoma sekondari kwa ufadhili.

Miaka ilivyopita Asha alifanikiwa kuwa mwalimu. Alirudi kijijini na kuanzisha kituo cha kusaidia watoto kusoma bure baada ya masomo. Alisema

 “Nilisaidiwa sasa ni zamu yangu kuwasaidia wengine.”

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments