Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Kulikuwa na Bata aliyeishi karibu na mto na huko msituni aliishi Mbweha aliyekuwa mjanja lakini mlafi sana. Kila siku Mbweha alifikiria njia ya kumkamata Bata ili amle.
Siku moja Mbweha alimwendea Bata akiwa na tabasamu akamwambia.
“rafiki yangu Bata mbona unaishi peke yako? Njoo tucheze msituni huko ni pazuri sana!”
Bata alimtazama Mbweha na akatambua kuwa ana nia mbaya. Akatumia akili yake na kusema.
“Sawa lakini kabla hatujaenda tufanye mashindano. Kila mmoja aoneshe kile anachoweza vizuri. Mimi nitazama ndani ya maji wewe ukae juu ya mti. Yeyote atakayeogelea au kupaa vizuri zaidi ndiye mshindi.”
Mbweha akakubali haraka bila kufikiri. Bata akaingia majini na kuogelea kwa ustadi akacheza juu ya maji bila wasiwasi. Wanyama wengine walimshangilia.
Ilipofika zamu ya Mbweha alijaribu kupanda mti kwa nguvu zote lakini akateleza na kuanguka chini! Wanyama wakaanza kucheka, na Bata akasema kwa utulivu.
“Kila kiumbe ana kipawa chake. Ukijaribu kutumia nguvu bila akili unaweza kuumia.”
Mbweha alipata aibu na akaondoka kimya kimya akijifunza kuwa ujeuri na tamaa mbaya huleta fedheha.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872
Post a Comment