BABA ALIYESAHAU THAMANI YA NYUMBANI

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Kulikuwa na baba mmoja aitwaye Hamisi. Kila siku alikuwa akitoka asubuhi na mapema kwenda mjini kufanya biashara. Alikuwa akisema:

 “Nafanya kazi kwa bidii ili familia yangu wawe na maisha mazuri.”

Lakini kwa bahati mbaya alizoea kukaa muda mwingi na marafiki akicheka nao, akinywa chai na kuhadithia mambo ya mjini. Akawa anarudi nyumbani usiku sana wakati mke na watoto wamelala.

Mtoto wake mdogo Sada alikuwa anamuandalia mchoro kila siku akitumaini atamwonyesha baba yake. Lakini baba aliporudi usiku alikuwa amechoka sana hata haangalii mchoro huo.

Siku moja Sada hakupiga kelele wala kucheza alikaa kimya tu. Mama yake akasema kimoyo moyo.

“Sada anaanza kujisikia vibaya kama hana baba.” Na Baba Sada alivyorudi nyumbani mama Sada alimwambia Baba Sada Hali anayopitia Mtoto wao.

Maneno hayo yalimgusa Hamisi moyoni zaidi ya kitu chochote. Siku iliyofuata hakukaa mjini muda mrefu. Alirudi mapema kuliko kawaida.

Alipofika Sada alikimbia kwa furaha akasema:

 “Baba leo umefika kabla ya giza! Angalia mchoro wangu!”

Hamisi alikumbatia mtoto wake moyo wake ukafurahi zaidi kuliko alipokuwa mjini akicheka na marafiki.Akatambua kwamba pesa na marafiki wa mjini ni kitu cha muda lakini familia ni ya kudumu.

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments