Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Nyanya ni tunda linalotumiwa sana katika familia nyingi kama kiungo muhimu cha chakula. Licha ya kuwa chanzo kizuri cha vitamini na madini nyanya pia ina tindikali. Tindikali hizi ndizo zinazosababisha ladha ya uchachu katika nyanya na huchangia pia harufu yake ya kipekee.
Tndikali kwenye nyanya pia inaweza kuwa na athari hasi kwa baadhi ya watu. Wale wenye matatizo ya tumbo kama vidonda au kiungulia wanaweza kuhisi maumivu au usumbufu wanapokula nyanya mbichi. Uchachu wake unaweza kuongeza tindikali tumboni na kusababisha hisia ya kuungua kifuani.
Vilevile kwa watoto wadogo tindikali hii inaweza kusababisha tumbo kujaa gesi au kuharisha ikiwa nyanya zitatumiwa mbichi bila kupikwa. Ndiyo maana wataalamu wa lishe wanashauri nyanya ipikwe kwanza ili kupunguza ukali wa tindikali kabla ya kumpa mtoto mdogo.
Pamoja na changamoto hizo ndogo nyanya bado inabaki kuwa chakula chenye umuhimu mkubwa. Tindikali yake inapodhibitiwa vizuri husaidia mwili kuwa na usawa wa asidi na alkali. Pia tindikali hizi husaidia kuzuia ukuaji wa bakteria hatari kwenye chakula hivyo kuongeza usalama wa chakula. Nyanya inapopikwabtindikali hupungua lakini bado inabaki na virutubisho muhimu vinavyoilinda miili yetu dhidi ya magonjwa.
Tndikali inayopatikana kwenye nyanya ni sehemu muhimu inayochangia ladha afyya ya mwili na usalama wa chakula. Ingawa inaweza kusababisha usumbufu kwa watu wachache.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872
Post a Comment