AMINA NA RAFIKI YAKE SUNGURA

 

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Siku moja Amina alipokuwa akienda kuteka maji mtoni alisikia sauti ndogo ya mnyama ikilia

"Kiiii… kiii… nisaidie!"

Amina alisimama na kuanza kutazama huku na huko. Mara akamwona sungura mdogo akiwa amenasa kwenye mtego uliowekwa na wawindaji.

 “Usiogope nitakutoa,” Amina alisema kwa upole.

Kwa uangalifu mkubwa alimfungua sungura yule. Sungura alimwangalia Amina kwa macho ya shukrani na kusema kwa sauti ya ajabu.

 “Asante sana wewe ni rafiki wa kweli. Nitakulipa wema wako.”

Amina alishangaa kusikia mnyama akiongea lakini akatabasamu na kumwacha sungura aende zake.

Baada ya siku chache Amina alipokuwa akicheza karibu na msitu alisikia ngurumo na kuona chui mkubwa akija kwa kasi kuelekea kwake. Amina alihisi hofu lakini kabla hata hajakimbia ghafla sungura yule yule alitokea pamoja na wanyama wengine wa msituni.

Walianza kupiga kelele na kuruka huku na huko wakimchafua chui hadi akapoteza mwelekeo na kukimbilia msituni. Amina alinusurika!

Sungura alimwambia Amina “Ulionesha wema bila kutarajia malipo. Wema siku zote hurudi kwa njia ya ajabu.”

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments