WEMA MDOGO UNAWEZA KULETA MIUJIZA MIKUBWA

 Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids


Siku moja jua lilipokuwa linang'aa angani Hawa msichana mchangamfu na mkarimu kutoka kijiji cha Mirimani alitoka kwenda kutafuta maua msituni. Akiwa karibu na mto aliona kitu kinang'aa juu ya jani kubwa.


Alipokaribia alikuta kipepeo wa dhahabu akiwa amekwama kwenye wavu wa buibui. Mabawa yake yalikuwa mazuri kama dhahabu inayong'aa jua likiwaka. Hawa aliinama polepole na kusema:


“Usijali nitakuokoa.”


Kwa mikono ya upole aliondoa nyuzi za buibui na kumwachilia kipepeo huyo. Kipepeo akapeperusha mabawa yake kisha akaruka juu angani lakini kabla hajaenda mbali alizunguka mara tatu juu ya kichwa cha Hawa na kutoweka kwa mwanga wa ajabu.


Usiku huo Hawa aliota kipepeo akimwambia “Wema wako hautasahaulika. Kuanzia kesho, kila unapotembea, maisha yatachanua.”

Asubuhi ilipofika Hawa alipokuwa akitembea kuelekea kisimani kila alipokanyaga ardhini maua ya rangi mbalimbali yalikuwa yanachanua mara moja. Watu wote wa kijijini walimfuata kwa mshangao.


Kuanzia siku hiyo kijiji chote kilimpenda Hawa. Walimuita “Msichana wa maua.”


Na kila alipopita maua na furaha vilimfuata nyuma yake.


emakulatemsafiri@gmai

l.com


0653903872


0/Post a Comment/Comments