WEMA HAUPOTEI KAMWE


Emakulata Msafiri

Kulikuwa na mwanamke mmoja mjane aitwaye Mama Amina ambaye aliishi kijijini na binti yake mdogo aitwaye Neema. Mama Amina alikuwa maskini lakini alikuwa na moyo wa upendo na hekima kubwa. Kila siku alifundisha Neema maadili mema kama vile kusema kweli, kusaidia wengine na kuwa na subira.

Siku moja walipokuwa wakitembea msituni kutafuta kuni Neema aliona ndege mdogo aliyejeruhiwa. Alichukua ndege huyo kwa upole na kumpeleka nyumbani. Mama yake alimsaidia kumtibu ndege huyo kwa kutumia majani ya dawa za kienyeji. Baada ya siku tatu ndege huyo alipona na akaruka juu akasema kwa sauti ya ajabu.

 “Asanteni kwa wema wenu! Nitawalipa kwa moyo wenu wa huruma. Fuateni mwanga wa jua kesho asubuhi utawaongoza hadi kwenye zawadi ya thamani.”


Asubuhi iliyofuata Neema na mama yake walifuata mwanga wa jua kama walivyoelekezwa. Walitembea hadi sehemu ya msitu ambayo hawakuwa wamewahi kufika. Ghafla Neema aliona mti wa dhahabu unaong’aa kwa mwanga wa ajabu. Chini ya mti huo kulikuwa na kikapu kilichojaa chakula, nguo nzuri na sarafu za dhahabu.

Mama Amina alitazama juu na kusema “Wema haupotei. Ukifanya mema yatakurudia.”

Tangu siku hiyo maisha yao yalibadilika. Walitumia mali yao kusaidia wengine kijijini. Neema alikua msichana mwenye busara na hadithi yake ya wema ilienea kote.

 

 

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872

 

 

 

0/Post a Comment/Comments