WAZAZI WETU NI KAMA MTI


Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Kulikuwa na mti mkubwa katikati ya kijiji. Watoto wote walipenda kucheza chini ya mti huu kwa sababu ulikuwa na kivuli kizuri na matunda matamu. Kati ya watoto wote kulikuwa na kijana mmoja aliyekuwa rafiki mkubwa wa mti huu. Kila siku alikuja kukaa chini ya mti kula matunda kupumzika na kulala kwenye kivuli chake.

Miaka ikapita kijana akawa mkubwa Siku moja alikuja kwa huzuni na kumwambia mti:

 "Nimekua sasa Nataka kusafiri na kuona dunia lakini sina pesa."

Mti akamwambia "Chukua matunda yangu yauze sokoni  utapata pesa."

Yule kijana alifanya hivyo na akaondoka kwa miaka mingi.

Baada ya muda mrefu alirudi akiwa mtu mzima. Alikuwa na huzuni tena.

 "Nimeoa sasa " alisema na nahitaji kujenga nyumba kwa familia yangu."

Mti akajibu kwa upendo  "Kata matawi yangu na mitini yangu tumia kujenga nyumba."

Mtu yule alifanya hivyo na akaondoka tena.

Miaka mingi ikapita akarudi akiwa mzee sana. Akasema "Nimechoka Sina kazi tena sina nguvu. Nahitaji mahali pa kupumzika."

Mti sasa ulikuwa umekauka hauna majani wala matunda. Lakini uliinua kichwa polepole na kusema "Sina kitu cha kutoa tena... lakini bado nina shina langu la zamani. Njoo kaa juu yake upumzike."

Yule mzee alikaa kwenye shina la mti na kupumzika kwa furaha.

 

 

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872

 

 

0/Post a Comment/Comments