Emakulata Msafiri
Kulikuwa na kijiji kidogo kinachoitwa Lembeni ambacho kilijulikana kwa amani na mshikamano wa kifamilia. Katika kijiji hicho aliishi kijana mmoja aitwaye Tindo mtoto wa pekee wa Bwana na Bi. Ndege. Wazazi wake walimpenda sana na walifanya kila wawezalo kuhakikisha anapata elimu nzuri na maisha mema.
Lakini kadri Tindo alivyoendelea kukua alianza kuwa mjeuri. Hakusikiliza wazazi wake alijibu kwa ukali na mara nyingine hata kuwatukana wazazi wake alipokatazwa kufanya mambo mabaya kama kuendekeza michezo ya kamari, kushinda mitaani au kutohudhuria shule.
“Mimi si mtoto mdogo tena! Mniachie nifanye ninachotaka!” alikuwa akisema kwa sauti ya dharau
Wazazi wake walihuzunika sana. Walijaribu kumkemea kwa upole na hata kumpeleka kwa viongozi wa dini na wazee wa kijiji lakini Tindo alizidi kuwa mbaya.
Siku moja Tindo alikataa kwenda shule na badala yake akaamua kwenda mjini akiamini maisha bora yanapatikana huko. Alitoroka usiku bila kuwaaga wazazi wake. Mjini mambo hayakuwa kama alivyotarajia. Alikutana na watu wabaya waliomtumia kufanya uhalifu. Alikamatwa na polisi na kufungwa.
Wakati akiwa gerezani alikumbuka maneno ya baba yake:
“Usipowaheshimu wazazi wako dunia pia haitakuheshimu.”
Baada ya miaka mitatu aliachiliwa. Alirudi kijijini kwa aibu na huzuni. Lakini wazazi wake walimpokea kwa upendo mkubwa. Alilia na kuwaomba msamaha.
Tangu siku hiyo Tindo alibadilika kabisa. Alijifunza kuwa unyenyekevu, utii na heshima kwa wazazi ni msingi wa maisha yenye baraka.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872
Post a Comment