Utapiamlo ni hali ya mtoto kukosa chakula bora chenye virutubisho muhimu vinavyohitajika mwilini ili awe na afya njema. Hili ni tatizo kubwa linalowaathiri watoto wengi hasa katika nchi zinazoendelea kama vile Tanzania, Kenya, na nchi nyingine za Afrika.
Mtoto anayepata utapiamlo hukosa nguvu mwilini, hukua kwa mwendo wa polepole na huwa dhaifu zaidi ya watoto wa umri wake. Baadhi ya watoto hupata maradhi kama vile kwashiorkor, ambapo tumbo huvimba na ngozi hubadilika rangi. Wengine hupatwa na marasmus ambapo mwili hukonda sana na kukosa mafuta kabisa.
Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa tarehe 11 septemba 2025 linalohusika na masuala ya watoto UNICEF imeeleza kuwa asilimia 13.5 ya watoto waliopimwa walibainika kuwa na utapiamlo mkali ikilinganishwa na asilimia 8.3 mwezi Julai. Hali ni mbaya zaidi katika eneo la Gaza City ambako njaa imethibitishwa na mtoto mmoja kati ya watano ameathirika.
UNICEF imesema watoto 12,800 waligunduliwa kuwa na utapiamlo mwezi Agosti. Hata hivyo idadi hiyo inaweza kuwa kubwa zaidi kutokana na kupungua kwa idadi ya watoto waliopimwa, baada ya vituo 10 vya matibabu kufungwa Gaza City na Kaskazini mwa Gaza kufuatia mashambulizi na maagizo ya kuhamishwa.
Aidha sehemu kubwa ya watoto waliolazwa wanakabiliwa na unyafuzi hali iliyo ongezeka maradufu tangu mwanzo wa mwaka huu 2025.
emakulatemsafiri@gmail.com
0654903872
Post a Comment