USIMDHARAU MTU KWASABABU YA UDHAIFU WAKE

 


Emakulata Msafiri

Siku moja katika msitu mkubwa kulikuwa na sungura mwepesi sana na kobe mwenye mwendo wa polepole. Sungura alipenda kujisifia kila wakati kuwa hakuna mnyama yeyote anayemshinda kwa mbio.

“Mimi ni mwepesi kama upepo!” alijigamba sungura mbele ya wanyama wengine wote.

Kobe alimwambia, "Lakini hata kwa polepole bado naweza kufika ninapokwenda. Unataka tufanye mashindano ya mbio?”

Sungura alicheka sana. “Wewe? Mashindano ya mbio na mimi? Hii itakuwa rahisi sana!”

Wanyama wote walikusanyika kushuhudia mashindano hayo. Mashindano yalianza!

Sungura alikimbia kwa kasi sana lakini baada ya muda mfupi aliona kobe bado yuko nyuma sana. Akaamua kupumzika chini ya mti akisema, “Nitapumzika kidogo bado nina muda mwingi wa kumshinda kobe.”

Lakini alipolala usingizi, kobe aliendelea kutembea polepole, bila kusimama.

Hatimaye sungura alipoamka alikimbia kwa haraka lakini akakuta kobe ameshafika mwisho wa njia.

Wanyama wote wakashangilia “Hongera Kobe!”



emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments