USILIPE UBAYA KWA UBAYA


Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Zamani za kale kulikuwa na rafiki wawili Kuku na Sungura. Waliishi kijiji kimoja na walipenda kucheza pamoja kila siku.

Siku moja Sungura alimwambia Kuku “Twende shambani tukatafute matunda.” Kuku alikubali haraka. Walipofika shambani wakaona matunda mengi mazuri.Sungura akasema “Tukishavuna,

tutagawana sawa sawa.” Wakaokota matunda hadi vikapu vikajaa. Lakini waliporudi kijijini Sungura akaanza kula matunda bila kusubiri Kuku.


Kuku alihuzunika lakini hakusema neno. Alipofika nyumbani akaweka matunda yake vizuri na kumshukuru Mungu. Kesho yake mvua kubwa ilinyesha. Matunda ya Sungura yote yakaharibika kwa maji kwa sababu hakuyatunza.

Sungura akaenda kwa Kuku kumuomba msaada. Kuku alimkaribisha na kumpa matunda kidogo. Sungura alijifunza kuwa na uvumilivu na kushirikiana na wenzake.

 

 

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872

0/Post a Comment/Comments