Emakulata Msafiri
Tiko alikuwa fisi mdogo aliyeishi peke yake kando ya msitu mkubwa. Alikuwa na manyoya ya kijivu na macho makubwa ya mng’ao. Wanyama wengine walimchukulia kuwa mnyonge, mwoga na asiyefaa chochote.
Lakini Tiko alikuwa na ndoto kubwa alitaka kuwa shujaa wa msitu. Wanyama Wakubwa
Kila siku Tiko alitazama simba, tembo na chui wakipita kwa majivuno. Alijaribu kujiunga nao lakini walimcheka.
"Wewe ni nani? Fisi mdogo tu! Tiko tu!" walimwambia.
Tiko hakukasirika. Alijua kuwa ndoto yake ilikuwa halisi hata kama wengine hawakuona hivyo.Siku moja mvua kubwa ilinyesha usiku kucha. Asubuhi mto ulio karibu na msitu ulifurika. Kambi ya wanyama ilifunikwa na maji. Wanyama walikimbia kila upande.
Ndama mdogo wa twiga alikwama juu ya jiwe maji yakimzunguka. Wanyama wote waliogopa kumsaidia hata simba!
Lakini Tiko hakusita. Alikimbia hadi mtoni, akatengeneza daraja kwa kutumia migomba iliyoanguka.
Akapita juu ya maji akamvuta ndama polepole hadi salama. Wanyama walishangaa! Simba alimtazama Tiko kwa mshangao, akasema:
"Tiko... wewe si mdogo tena. Wewe ni shujaa."
Tangu siku hiyo, hakuna aliyemwita “Tiko tu” tena. Alijulikana kama Tiko Shujaa. Alifundisha wanyama kuwa ujasiri haupimwi kwa ukubwa wa mwili bali kwa ukubwa wa moyo.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872
-
Post a Comment