Emakulata Msafiri
Siku moja kulikuwa na tembo mdogo aitwaye Timo. Timo aliishi msituni pamoja na wanyama wengine kama vile twiga, fisi, pundamilia na sungura. Ingawa Timo alikuwa mkubwa kuliko wote alikuwa mnyenyekevu na mwenye moyo wa upendo.
Siku moja msitu ulikumbwa na ukame. Mito ilikauka na chakula kilianza kupungua. Wanyama wakaanza kuwa na hofu.
Timo alifikiria kwa muda kisha akasema "Nimewahi kusikia kutoka kwa bibi yangu kuwa kuna chemchemi ya maji mbali kidogo lakini tutaweza kuipata tukisaidiana."
Wanyama wote walikubaliana. Twiga alitumia shingo yake ndefu kuona njia kutoka juu ya miti sungura aliangalia mashimo madogo yenye maji na Timo alibeba wanyama wadogo waliokuwa wamechoka.
Baada ya safari ndefu walifika kwenye chemchemi ya maji safi! Wanyama walishangilia na kunywa maji kwa furaha. Waligundua kuwa kwa kushirikiana wanaweza kushinda changamoto yoyote.
Tangu siku hiyo Timo na marafiki zake waliishi kwa amani wakisaidiana kila wakati.
Post a Comment