TAMAA YA WAGOMBANISHA MARAFIKI


Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Siku moja Mbwa na Paka waliishi pamoja nyumbani kwa bibi mmoja mkarimu. Bibi huyu alikuwa akiwapikia chakula kitamu kila siku. Lakini siku hiyo bibi alitoka kwenda sokoni na akasahau kuwaachia chakula.

Njaa ilipoanza kuwasumbua Mbwa akamwambia Paka  "Sisi ni marafiki twende jikoni tuangalie kama kuna mabaki ya chakula."

Walipofika jikoni waliona kipande kimoja tu cha nyama kilichobaki mezani. Mara moja wote wakakitaka.

Paka akasema "Mimi ndimi niliyekiona kwanza kwa hiyo ni changu."

Mbwa akajibu "Lakini mimi ni mkubwa kuliko wewe na nina njaa zaidi!"



Wakaanza kugombana na kurushiana maneno. Kelele zao zilimfanya Sungura jirani yao aje kuangalia kilichotokea. Sungura akasema  "Mna nini nyie? Kwa nini mnapigania kipande kimoja cha nyama?"

Walipomweleza Sungura alifikiri kisha akasema "Hebu nilete mizani. Nitagawanya kipande hicho sawa kwa nusu."

Alichukua kipande cha nyama akakigawanya. Lakini upande mmoja ukawa mkubwa zaidi. Sungura akauma kula upande mkubwa kidogo ili visawiane. Kisha upande wa pili ukawa mkubwa akauma kula tena. Hadi kipande cha nyama kikawa kidogo sana na hakuna kilichobaki kwa Mbwa wala Paka!

Wote wakasema kwa sauti "Ohoo! Sasa tumebaki bila chochote!"

Sungura akawa ameshiba na kutabasamu kisha akaondoka.

 

 

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872

 

 

0/Post a Comment/Comments