POLEPOLE NDIO MWENDO

 Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Kobe alikuwa akiishi kando ya mto. Alikuwa mnyama mdogo mwenye gamba zito na hakukimbia haraka kama wanyama wengine. Wanyama wengi walimcheka wakisema.

"Wewe ni mvivu huwezi kufika mbali!"

Lakini kobe hakuwajibu moyo alitabasamu na kujisemea moyoni kila jambo Lina mwisho wake Alijua jambo moja uvumilivu hushinda haraka.

Siku moja kulikuwa na ukame mkubwa maji ya mto yakaanza kukauka. Wanyama wenye mbio walikimbia kwa hasira wakitafuta maji lakini walichoka na kurudi bila kupata. Kobe akaamua kuanza safari polepole kuelekea upande mwingine wa msitu ambako alisikia kuna ziwa dogo.

Alitembea siku moja, mbili, tatu… bila kukata tamaa. Hatimaye alifika kwenye ziwa lenye maji mengi. Wanyama waliokuwa wamemcheka walimfuata na kunywa maji kwa furaha.

Wote wakasema "Kweli kobe umetuokoa kwa uvumilivu wako hakika hatutasahau hiking kitendo ulichotufanyia Sisi sote."

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments