MTOTO ALIYEBADILISHA SHULE

 Emakulata Msafiri

Amani aliporudi nyumbani kutoka shule alimkuta mama yake akiwa na boksi dogo juu ya meza. Alifungua macho kwa mshangao.

“Mama hii ni nini?” Amani aliuliza.

“Zawadi yako kwa kufanya vizuri darasani!” Mama alijibu kwa tabasamu. Amani alifungua boksi kwa haraka. Ndani kulikuwa na simu mpya kabisa ya kisasa!

“Wooooow! Hii ni simu ya tekno asante sana mama!” Amani aliruka kwa furaha. Siku iliyofuata Amani aliichukua simu shule kwa siri. Walimu walikataza wanafunzi kwenda na simu lakini Amani alitaka kujionesha kwa marafiki.

Alipoifikisha darasani watoto wote walikusanyika kumuona. “Hebu tucheze nayo muda wa mapumziko!” alisema rafiki yake Kito.

Wakati wa mapumziko Kito alichukua simu na kuanza kucheza nayo. Kwa bahati mbaya simu ilianguka na kioo kikapasuka!

“Aiyaa! Kimevunjika!” Amani alipiga kelele. Wote walinyamaza. Kito alimtazama Amani kwa hofu.

“Samahani Amani... sijakusudia.”

Amani alihisi kulia lakini akavuta pumzi. Badala ya kumlaumu Kito au kusema uongo kwa mama aliamua kuwa mkweli. Alipofika nyumbani alimwambia mama kilichotokea.

“Mama simu imevunjika. Nilikiuka sheria ya shule na nikaichukua. Samahani...”

Mama alimtazama Amani akasikitika kidogo kisha akasema: “Umefanya makosa lakini umeonesha ujasiri na uaminifu kwa kusema ukweli. Nitakusaidia kuirekebisha lakini utaiweka mbali hadi utakapojifunza kuwajibika.”

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments