Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Palikuwa na mji wa ajabu uitwao Chekechea mahali ambapo wanyama waliishi pamoja kwa amani. Lakini kulikuwa na jambo moja la kushangaza hakuna aliyewahi kucheka.
Ndiyo hakuna aliyepiga kicheko hata siku moja! Simba, twiga, fisi, paka hata tumbili wote walitembea tu wakiwa na nyuso za huzuni. Walifanya kazi, walikula, walilala lakini hawakufurahia chochote.
Lakini Walikuwa wamesahau kabisa jinsi ya kucheka.
Siku moja alifika mgeni kutoka mbali. Alikuwa ni mtoto wa binadamu aliyepotea msituni baada ya kuenda kupanda milima na wazazi wake.
Alipofika mji wa Chekechea aliona kuwa kila mmoja alionekana mnyonge. Alimwendea twiga na kusema:
“Habari Twiga! Nitakuchekesha!”
Akajipinda na kucheza kama ng’ombe anayecheza dansi ya nyuki. Twiga alimtazama tu hakucheka.Akamwendea fisi na kuigiza sauti ya simba akisema kwa sauti nyembamba
“Mimi ni simba mfalme wa vicheko!”
Lakini fisi alitabasamu kidogo tu bado hakupiga kicheko.
Hakukata tamaa. Alikusanya wanyama wote katikati ya mji na akaanza kuimba wimbo wa kuchekesha akiwa anacheza vibaya makusudi akidondoka dondoka, akajipaka matope kisha akapiga kiki kama kuku aliyevaa viatu vya tembo.
Kwa mara ya kwanza tumbili alicheka.Kisha paka akaungana naye Kisha fisi akacheka kwa sauti kubwa sana, mpaka akaanguka chini.
Na hatimaye mji mzima ukatiririka kwa sauti za kicheko.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872
Post a Comment