MIGUU YENYE VUMBI AKILI ILIYONG'AA


Emakulata Msafiri

“Mama sitaki kwenda shuleni tena!” Sara aliingia chumbani akiwa amekasirika machozi yakimlenga lenga.

Mama yake ambaye alikuwa ameanza kukaanga maandazi ya asubuhi alizima jiko na kuketi naye.

 “Kwani nini tena mwanangu?”

Sara alinyamaza kisha akasema kwa sauti ya chini:

 “Wananicheka. Wanasema viatu vyangu vimechanika na gauni langu ni la zamani. Jana waliniita maskini mbele ya wanafunzi wote…”

Mama yake hakusema kitu mara moja. Alimkumbatia tu kwa nguvu ya upendo ambayo haileweki kwa maneno. Halafu kwa sauti tulivu alisema:


“Usijali kuhusu walichosema. Hawaoni bidii yako. Hawajui umeamka saa kumi alfajiri kila siku. Lakini mimi najua. Na najua siku moja utavaa viatu utakavyovitaka na hakuna atakayekuona kama masikini tena  kwa sababu utakuwa na maisha yako mikononi mwako.”

Siku hiyo Sara alienda shuleni bila kusema neno. Lakini moyoni aliamua kitu: Atasoma kwa bidii zaidi kuliko wote.

Miaka kadhaa baadaye akiwa kwenye jukwaa la chuo kikuu kupokea tuzo ya mwanafunzi bora wa kitaifa alikumbuka siku hiyo. Alikumbuka viatu vya plastiki. Alikumbuka maneno ya mama yake na alitabasamu.

 

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872

0/Post a Comment/Comments