Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Mchezo wa sarakasi ni mojawapo ya michezo ya kuvutia sana kwa watoto. Sarakasi humaanisha kufanya mazoezi au maonesho ya ajabu ajabu kama vile kuruka juu, kusimama kwa mikono, kucheza kwenye kamba ya juu au kuzunguka kwa gurudumu bila kuanguka.
Mara nyingi michezo ya sarakasi huchezwa kwenye maonesho ya burudani kama tamasha au siku ya michezo shuleni. Watoto huvaa mavazi ya rangi nyingi na hupaka nyuso rangi au kuvaa nyuso za vikaragosi (maski). Wengine hucheza kama wanyama kama simba, tembo au nyani. Hii huwafanya watazamaji kucheka na kufurahi sana.
Katika shule yetu tuliwahi kuwa na tamasha la sarakasi siku ya wazazi. Watoto walifanya maajabu! Wengine walikuwa wakizunguka juu ya magurudumu bila kushikwa wengine waliruka kwa minyoo na baadhi walifanya vituko vya kuchekesha kama wajanja wa vikaragosi. Wazazi walishangilia kwa makofi na vigelegele!
Mchezo wa sarakasi unafaa sana kwa watoto kwa sababu Huwasaidia kuwa na mafanikio ya mwili kama uimara, wepesi na usawa. Huwajengea ujuzi wa kushirikiana na wenzao.
Hata hivyo mchezo huu unahitaji tahadhari. Watoto hawapaswi kujaribu sarakasi za hatari bila msaada wa mwalimu au mtu mzima. Lazima wavae mavazi salama na wafanye mazoezi ya kutosha kabla ya kuonesha mbele za watu
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872
Post a Comment