MAJIVUNO HUPOTEZA MALENGO

 

Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Siku moja kulikuwa na sungura mdogo anayeitwa Tiko.Tiko alikuwa na marafiki wengi lakini alikuwa anapenda sana kujisifu kuwa yeye ni mwepesi kuliko wanyama wote.

Siku moja alipomwona kifaru mkubwa akitembea polepole alicheka na kusema

"Wewe Kifaru polepole kama kobe! Unaweza kunishinda kwenye mbio kweli?"

Kifaru akatabasamu tu na kusema

"Sijawahi kukimbia mbio lakini tukijaribu huenda ukashangaa."

Wakapanga mashindano ya kukimbia kesho yake. Wanyama wote wa msitu walikusanyika kushuhudia.

Alama ya kuanza ilipopigwa Tiko alienda mbio kama upepo. Alipofika katikati ya njia aliona hana mpinzani karibu akasema:

 "Aah hebu nilale kidogo. Huyu kifaru atachukua miaka kunifikia."

Tiko alipofumbua macho akaona kifaru tayari ameshinda. Akajifunza kwamba uvumilivu na bidii ni muhimu kuliko mbio za haraka zisizo na mpango.

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872




0/Post a Comment/Comments