MADHARA YA MCHEZO WA KUVUTA KAMBA KWA WATOTO

Emakulata Msafiri

Mchezo wa kuvuta kamba ni mojawapo ya michezo ya kitamaduni ambayo imekuwa ikichezwa na watoto katika maeneo mbalimbali duniani hasa vijijini. Ingawa mchezo huu huonekana kuwa wa kufurahisha na unaohamasisha ushirikiano kati ya watoto.

Madhara ya moja kwa moja ya kimwili ni makubwa iwapo mchezo huu hautachezwa kwa tahadhari. Wakati wa kuvuta kamba watoto wengi huweka nguvu nyingi bila kuelewa mipaka ya miili yao. Hii inaweza kusababisha majeraha kama vile kuvunjika kwa mifupa, kuumia kwa mikono, mabega au hata mgongo. Watoto wengine huweza kuanguka na kuumia kichwa au viungo vingine muhimu mwilini.

Mchezo huu unaweza kuleta matatizo ya kijamii kati ya watoto. Kwa kuwa unahusisha ushindani mkali kati ya makundi mawili mara nyingine ushindani huu huweza kugeuka kuwa uhasama. Watoto waliopoteza huweza kujihisi kudharauliwa au kubezwa na wenzao hali inayoweza kusababisha migogoro ya kijamii, chuki au hata uonevu.

Kuna hatari ya kisaikolojia kwa baadhi ya watoto. Watoto wengine huwa na hisia nyepesi na hushindwa kuvumilia kushindwa au kuonekana dhaifu mbele ya wenzao. Kushindwa mara kwa mara au kutengwa kwa sababu ya udhaifu wao wa kimwili kunaweza kupunguza hali ya kujiamini na kuwafanya kujiona hawafai.

Ni wazi kuwa ingawa mchezo wa kuvuta kamba ni burudani kwa watoto pia unaleta madhara mbalimbali ya kimwili, kijamii na kisaikolojia. Ni wajibu wa jamii kuhakikisha kuwa watoto wanacheza kwa usalama na kwa maadili mema ili kufurahia faida za mchezo huu bila kupitia madhara yake. Michezo ni muhimu kwa ukuaji wa mtoto lakini lazima ichunguzwe na kuendeshwa kwa uangalifu mkubwa.


emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments