KILIO KUTOKA MLIMA WA AJABU

 


Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Kulikuwa kimoja chenye majani ya kijani kibichi na ndege wa kupendeza aliishi mtoto mmoja aliyejulikana na kila mtu si kwa wema wake bali kwa ujeuri wake. Jina lake aliitwa Baraka.

Baraka alikuwa na kila kitu chakula kizuri, nguo safi na wazazi waliompenda sana. Lakini alikuwa na kitu kimoja kilichomkosesha sifa hakuwa msikivu. Alipoambiwa safisha chumba, alijifanya hasikii. Alipoonywa asicheze karibu na ziwa alikimbilia huko kwa makusudi. Alipoambiwa asiwadharau wakubwa alicheka na kujifanya mjanja.

Wazee wa kijiji walimtazama kwa huzuni. Mama yake alijaribu kumrekebisha kwa upole baba yake alimtisha kwa fimbo lakini Baraka hakuwa tayari kubadilika.

Siku moja aliamka asubuhi na kusema kwa sauti kubwa “Leo nitakwenda kupanda mlima ule mkubwa nyuma ya kijiji ule mlima ambao watu wanasema una nyoka wa ajabu!”

Watu waliogopa. Wazazi wake walimuonya sana. Lakini Baraka alijibu kwa kejeli "Mimi siogopi hadithi za wazee!”

Alipofika mlimani aliona vitu vya kutisha na vikaanza kumkimbiza na asijue nini cha kufanya Baraka alikimbia huku Analia, nisaidieni!, nisaidieni!


Bahati nzuri, mzee mmoja wa kijiji ambaye alikuwa anakata kuni alimsaidia na Kwa kumrudisha nyumbani kwao.Alimrudisha nyumbani akiwa mchovu na mwenye majuto.

Tangu siku hiyo Baraka alibadilika kabisa. Alisalimia wakubwa, alitii wazazi wake na alikuwa wa kwanza kushauri watoto wenzake kuwa watii na wanyenyekevu.

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments