Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Aliishi bundi mmoja mwenye macho makubwa na manyoya ya rangi ya kahawia. Alikuwa akiishi kwenye shimo la mti mrefu katikati ya msitu. Bundi huyu aliitwa Bundi Mwerevu kwa sababu alijua mambo mengi kuhusu msitu na wanyama wote.
Wakati wanyama wengine walilala usiku Bundi Mwerevu aliamka. Kila usiku aliruka kimya juu ya miti akitazama nyota na kusikiliza sauti za msitu. Alipenda kutazama kila kitu kwa makini ili ajue kinachoendelea.
Siku moja moto mdogo ulianza msituni. Wanyama wengi walikuwa wamelala na hawakujua. Bundi Mwerevu aliona moshi ukinuka. Kwa sauti yake ya kipekee alianza kuita.
“Huu huu! Moto! Moto!”
Sauti yake iliwaamsha wanyama wote. Wote walikimbilia sehemu salama na moto ukazimwa mapema. Wanyama walimshukuru Bundi Mwerevu kwa kuwa macho wakati wengine wamelala.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872
Post a Comment