Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Zaki alikuwa na moyo mkubwa na alikuwa na tabia ya kusaidia wenzake kila alipoona wanahitaji msaada. Alikuwa na ndoto ya kuwa mchoraji maarufu lakini alikosa vifaa vya kuchora. Alikuwa na kalamu moja ya zamani na kipande kidogo cha karatasi.
Siku moja Zaki alipokuwa akichora kwenye kivuli cha mti mkubwa aliona kundi la watoto wakicheka na kumdharau kwa sababu alichora picha zisizo nzuri. Walimwambia "Hii picha yako ni mbaya sana! Utafanya nini na hiyo kalamu ya zamani?"
Zaki aliguswa sana na maneno hayo lakini hakujivunja moyo. Alijua kuwa kila mtu ana njia yake ya kufanikiwa. Alikumbuka kusema maneno aliyosikia kutoka kwa bibi yake "Ukitaka kufanikiwa lazima uwe na moyo wa dhati na usikate tamaa."
Hivyo Zaki alijitahidi zaidi na akaendelea kuchora kila siku. Aliamua kusaidia watoto wengine ambao walikuwa na shida ya kuchora akiwafundisha jinsi ya kutumia vifaa vya kawaida kutengeneza picha nzuri.
Muda ulivyoenda picha za Zaki zilianza kuwa nzuri zaidi na watu walikubali juhudi zake. Aliweza kuwa mchoraji maarufu lakini aliendelea kuwa na moyo wa kusaidia wengine. Alijivunia sio tu mafanikio yake bali pia uwezo wa kusaidia wengine kufikia ndoto zao.
Na hivyo Zaki alijifunza kuwa mafanikio hayaji kwa bahati tu bali kwa juhudi, subira na moyo wa kusaidia wengine.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872
Post a Comment