JE! NANI AWAJIBIKE KUSAIDIA WATOTO WA MTAANI?

Emakulata Msafiri

Katika mitaa ya miji mingi hasa mijini mikubwa kama Dar es Salaam au Nairobi tunaona watoto wadogo wakizurura barabarani wakiomba msaada wakilia, wakikimbiza magari, wakiomba chakula au pesa. Hawa ni watoto wanaojulikana kama watoto omba omba.

Sababu kuu zinazowasukuma mitaani ni umasikini, migogoro ya kifamilia au kupoteza wazazi. Wengi huishi maisha magumu, bila chakula cha kutosha, elimu, au huduma za afya.

Changamoto kubwa ni kwamba wanakosa ulinzi na haki zao huvunjwa mara kwa mara. Mara nyingi hukumbana na unyanyasaji, matumizi mabaya ya dawa za kulevya na hata kuingizwa kwenye vitendo vya kihalifu.


Ni jukumu la jamii, serikali na mashirika ya kijamii kuhakikisha watoto hawa wanapata msaada, elimu na malezi bora ili waweze kuwa raia wema na wenye mafanikio siku za usoni.

Watoto omba omba si tatizo tu bali ni kiashiria cha matatizo makubwa ya kijamii. Tukiwasaidia tunajenga taifa bora.

 

 

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872

 

 

0/Post a Comment/Comments