HAZINA ILIYOFICHWA SHAMBANI

 Emakulata Msafiri

Mwanakwetukids

Kulikuwa na kijana mmoja aliyeitwa Juma. Juma alipenda kulala na kucheza hakupenda kufanya kazi. Baba yake alikuwa na shamba kubwa lililohitaji kulimwa lakini Juma hakutaka kusaidia.

Siku moja baba yake akamwambia.

"Juma, kwenye shamba letu kuna hazina kubwa imefichwa. Ukiifanyia kazi utaipata."

Juma aliposikia neno hazina alifurahi sana. Akaamka mapema kila siku akalima shamba lote kwa bidii akifikiri atapata dhahabu au fedha.

Lakini baada ya kulima kwa muda mrefu hakupata kitu chochote. Akachoka na akamuuliza baba yake:

"Baba hazina iko wapi? Nimechimba kila sehemu!"

Baba akatabasamu na kusema,

"Hazina siyo dhahabu ni mazao utakayovuna kwa bidii yako shamba litatoa chakula kingi na utakuwa tajiri wa nafaka."

Kweli baada ya muda shamba lilijaa mahindi, maharage na viazi. Juma alijifunza kuwa bidii ndiyo hazina ya kweli.

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments