Emakulata Msafiri
Palikuwa na msichana mmoja mcheshi sana aitwaye Hawa. Aliishi kijijini na bibi yake na walikuwa na shamba dogo la mahindi.
Siku moja Hawa alipokuwa akilima shambani aliona mbegu moja ya mahindi yenye kung’aa kama dhahabu. Akaipanda haraka huku akisema:
"Wewe mbegu nikikupanda nipe maajabu siyo matatizo!"
Baada ya siku tatu mmea mmoja mkubwa ukaota lakini si kawaida! Kila jua linapochomoza mahindi yale yalikuwa yanaimba:
"Tunapenda jua, tunapenda mvua, Hawa ni rafiki yetu wa kweli wa shamba!"
Lakini siku moja kundi la kuku waliamua kwenda shambani. Waliwasikia mahindi wakiimba wakaona ni muziki wa kufurahisha. Wakaanza kucheza!
Kuku mmoja akasema “Hii ndiyo disco ya shamba! Tupige densi!”
Walicheza sana mpaka wakaangusha mimea yote. Hawa alipokuja alikuta kuku wamechoka na mahindi yamezimika kimya kabisa!
Hawa akauliza “Nani kavunja mahindi yangu?”
Hawa alicheka tu “Basi kesho turudi lakini mvalie vizuri siyo kuharibu shamba tena!”
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872
Post a Comment