Emakulata Msafiri
Mwanakwetukids
Hapo zamani za kale katika kijiji aliishi fisi mdogo aitwaye Filo. Filo alikuwa tofauti na fisi wengine alipenda kucheka sana! Kila kitu kwake kilikuwa cha kuchekesha ,ndege akiruka vibaya twiga akikohoa au hata kobe akitembea polepole.
Wanyama wengine walimshangaa."Mbona Filo anacheka kila mara? Maisha si mchezo!" walinong’ona.
Lakini Filo hakujali aliendelea kucheka na kuwafanya wengine wajisikie vizuri.
Siku moja mvua kubwa ilinyesha kwa siku tatu mfululizo. Mito ikafurika na mapango yakajaa maji wanyama wakaanza kuwa na hofu.
Walikusanyika chini ya mti mkubwa kujadili la kufanya. Wote walikuwa na huzuni na wasiwasi. Lakini ghafla Filo alisimama na kusema kwa sauti.
"Hata kama tuna shida hatuwezi kusahau kucheka kidogo!"
Akaanza kuigiza simba akiwa na kikohozi, akamwigiza tembo akijaribu kuruka kama ndege na wote wakaanza kucheka! Hata yule simba mkali alitabasamu kidogo.
Baada ya furaha hiyo fupi wanyama walipata nguvu mpya. Wakaanza kusaidiana kujenga sehemu salama ya kukaa hadi mvua iishe. Walitumia miti, majani na hata mawe kuzuia maji kuingia.
Na walipofanikiwa wote walimkumbatia Filo na kusema "Asante kwa kutufundisha kuwa hata wakati wa shida tabasamu linaweza kutupa nguvu!"
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872
Post a Comment