Emakulata Msafiri
Katika kijiji kimoja aliishi msichana mdogo shupavu aitwaye Doto. Alikuwa na hamu ya kugundua mambo mapya hasa hadithi alizokuwa akisikia za pango la mbweha mahali pa ajabu palipojaa siri na majaribio.
Siku moja Doto akaamua kwenda kulisaka pango hilo. Alijifunga mkoba wake akachukua maji, mkate na tochi kisha akaingia msituni kimya kimya.
Baada ya kutembea kwa muda alifika kwenye mlango mkubwa wa pango. Kulikuwa na maandishi yaliyosema:
“Hapa huingia wenye moyo wa kweli na nia safi.”
Doto akaingia bila kuogopa. Ndani ya pango palikuwa na mwanga wa ajabu na ghafla akatokea Mbweha Mwekundu mwenye macho ya kung’aa.
“Karibu Doto,” Mbweha alisema kwa sauti ya pole. “Ili uondoke salama jibu hili: Ni nini kilicho bora zaidi kuwa hodari au kuwa mwema?”
Doto akatafakari kisha akajibu, “Kuwa mwema kwa sababu wema huleta amani na marafiki.”
Mbweha alitabasamu na kusema “Jibu sahihi! Wewe ni wa pekee. Endelea kuwa mwenye moyo wa huruma.”
Doto alitoka pangoni akiwa salama na mwenye furaha. Alipoanza kurudi nyumbani alijua kuwa siri ya kweli haiko kwenye mapango bali kwenye moyo safi.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872



Post a Comment