Emakulata Msafiri
Palikuwa na kifaranga mdogo aliyekuwa akiishi na mama yake kuku pamoja na vifaranga wenzake kwenye kijiji kidogo kilichozungukwa na mashamba ya mahindi na miti mikubwa. Kifaranga huyo.alikuwa na udadisi mwingi na kila mara alitaka kujua mambo mapya.
Siku moja asubuhi mama yao aliwapeleka kuchakura chakula karibu na kichaka. Mama aliwaonya “Msitoke mbele zangu huku porini kuna hatari nyingi!” Vifaranga wote walitii isipokuwa mmoja. Aliona kipepeo mzuri akiruka kuelekea msituni na akashawishika kumfuata bila kusema kwa yeyote.
Alizidi kufuata kipepeo huyo huku akipita kwenye nyasi ndefu akavuka mto mdogo hadi akajikuta mahali pasipojulikana. Alipogeuka nyuma hakumuona mama wala vifaranga wenzake. Ghafla akatambua kuwa amepotea.
Alianza kulia “Mamaaaa! Mamaaaa!” Lakini hakuna aliyemjibu. Alihisi baridi na hofu ikamjaa. Aliendelea kutembea akitafuta njia ya kurudi lakini kila njia ilionekana kuwa mpya kwake. Ndege waliimba juu ya miti nyoka alipita karibu naye na paka mwitu alimtazama kwa tamaa lakini kwa bahati nzuri yule alijificha kwa haraka chini ya mwamba.
Wakati huohuo mama yake alikuwa akimtafuta kwa hofu kubwa. Aliita kwa sauti, “Totooo! Totooo!” Vifaranga wenzake walihuzunika pia. Baada ya saa kadhaa za kumtafuta mama kuku alimsikia kifaranga akilia kwa mbali. Alikimbia kwa haraka na kumkuta amejificha.
Mama! alipiga kelele kwa furaha na kukimbilia kumkumbatia mama yake. Mama yake alimuangalia kwa huruma na kusema “Nilikuonya usitoke mbele yangu. Dunia ya nje si salama kwa kifaranga mdogo kama wewe.”
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872
Post a Comment