USIOGOPE KUJARIBU TENA NA TENA

Emakulata Msafiri

Siku mojaTembo alienda kutembea mbali akitafuta matunda. Alikuwa anafurahia kula maembe, mapera na tikiti pori. Alivyokuwa anakula na kusonga mbele hakujua kuwa alikuwa akitoka kwenye njia ya kawaida ya msitu.

Baada ya muda alitambua kuwa amepotea.

“Eh! Niko wapi sasa? Sina hata harufu ya familia yangu!” alijisemea kwa huzuni.

Tembo alihangaika kutafuta njia ya kurudi. Alitembea mchana kutwa akavuka mito na milima lakini bado hakuiona njia ya kurudi nyumbani.

Lakini Tembo hakuacha kutafuta. Alikumbuka alama za miti alizokuwa anaziona karibu na nyumbani. Alianza kuzitafuta kwa makini akitumia masikio yake makubwa kusikiliza sauti za familia yake.

Baada ya siku mbili alisikia mlio wa ndovu wengine wakipiga kelele ilikuwa familia yake! Tembo alikimbia kwa furaha na kukutana nao tena. Wote walifurahi sana kumuona amerudi salama.


emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments