UMUHIMU WA KUSOMA VITABU KWA WATOTO

 

Emakulata Msafiri

Kusoma kitabu ni jambo muhimu sana kwa kila mtoto. Kitabu kinatufundisha mambo mengi mapya na hutufungulia milango ya maarifa. Mtoto anayesoma kwa bidii huweza kujifunza mambo ambayo hayatambui kwa kusikia tu au kuona kwenye runinga.

Kusoma kitabu husaidia kukuza akili za watoto. Watoto wanaosoma mara kwa mara hujifunza maneno mapya, wanajua hadithi mbalimbali na wanaweza kuelewa mambo kwa urahisi zaidi. Kusoma pia husaidia mtoto kuwa na fikra za ubunifu na kufikiri kwa haraka.

Aidha kusoma kitabu hutuandaa kwa maisha ya baadaye. Mtoto mwenye maarifa mengi ana nafasi kubwa ya kufanikisha ndoto zake. Kusoma kunasaidia watoto kuelewa dunia inayowazunguka tamaduni tofauti na hata kujifunza jinsi ya kushughulika na changamoto mbalimbali.

Kwa hiyo wazazi, walimu na watoto wenyewe wanapaswa kuweka muda wa kusoma kila siku. Kitabu si kitu cha kufurahisha tu bali ni rafiki wa maisha. Mtoto anayesoma kitabu anakuwa mtu mwenye maarifa na hekima.



emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments