Emakulata Msafiri
Katika mtaa mdogo wa jiji la Dar es Salaam aliishi msichana mdogo aliyeitwa Chiku. Chiku alikuwa na umri wa miaka kumi na alikuwa mwerevu sana. Alipenda shule na alitamani siku moja awe mtu wa kufanikisha mambo makubwa.
Familia ya Chiku haikuwa na pesa nyingi. Wazazi wake walifanya kazi ngumu lakini mara nyingi haikuwa rahisi kupata chakula cha kutosha kila siku. Chiku aliona huzuni usoni mwa mama na baba zake na alihisi moyo wake unauma.
Siku moja baada ya kurudi kutoka shuleni Chiku aliwaona wazazi wake wakizungumza kwa hofu. Baba yake alisema "Leo tumeshindwa kulipa kodi ya nyumba na pia chakula kinaanza kuisha." Chiku alihisi moyo wake ukipiga nguvu na akajua kuwa lazima afanye jambo.
Alikumbuka kwamba karibu na shule kulikuwa na soko la matunda na watu wengi waliuza matunda lakini kwa bei kubwa. Chiku alifikiria “Naweza kuuza matunda kidogo kwa bei nafuu na kupata pesa za kununua chakula kwa familia.”
Siku hiyo hiyo Chiku alikwenda kwa mzee mmoja aliyekuwa mkulima wa matunda karibu na mtaa wao. Alimwomba mzee huyo amuuze matunda kwa bei ya chini. Mzee huyo aliyeitwa Babu Mzee alimsikiliza kwa upole na kusema “Chiku ninafurahi kuona moyo wako wa kusaidia familia. Nitakupatia matunda kwa bei nafuu.”
Chiku alifurahi sana. Alirudi nyumbani na kuanza kupanga biashara yake. Aliweka meza mdogo karibu na shule na kuanza kuuza matunda aliyoyapata kutoka kwa Mzee.
Wanafunzi walianza kununua kutoka kwake kwa sababu matunda yake yalikuwa safi ya bei nafuu na Chiku alikuwa na tabasamu la kupendeza kila wakati alipowahudumia. Alijua kuwa jambo hili lilikuwa zamu yake kusaidia familia yake.
Baada ya miezi kadhaa, biashara ya Chiku ilikua kubwa zaidi. Aliweza hata kusaidia watoto wengine mtaani kwa kuwasaidia kupata chakula na vifaa vya shule.
Wazazi wake walijivunia sana Chiku na mtaa mzima ulimpenda kwa moyo wake wa huruma bidii na upendo kwa watu.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872
Post a Comment