Emakulata Msafiri
Kila mtu anahistoria yake katika maisha, kulikua na msitu mkubwa wa Mti Mkavu waliishi wanyama wengi. Simba ndiye alikuwa mfalme wa msitu akiheshimiwa na wote kwa nguvu na busara zake. Lakini kulikuwa na fisi mmoja mjanja aliyeitwa Kileo aliyependa ujanja kuliko ukweli.
Siku moja simba aliugua ghafla na kulala pangoni kwake akiwa dhaifu. Wanyama wote walikusanyika kujadili namna ya kumsaidia mfalme wao. Kileo akiwa na tamaa ya kutawala aliwashauri wanyama waseme kuwa Simba amekufa ili achukue ufalme.
Lakini Sungura alipinga wazo hilo. Akasema, “Hatutakiwi kumgeuka mfalme wetu. Tumsaidie apone kwani ametutunza miaka yote.” Wanyama wengine wakakubaliana na Sungura.
Walichanga matunda mazuri, asali na dawa kutoka kwa Daktari Kobe wakavipeleka kwa Simba kila siku. Baada ya siku tatu Simba akapata nguvu na akatoka pangoni.
Alipoambiwa yote yaliyotokea simba alitabasamu na kusema:
“Asanteni kwa uaminifu na ushirikiano wenu. Msitu huu utadumu salama sababu ya mioyo yenu safi.”
Kisha akamgeukia fisi Kileo na kumwambia “Ujanja huzaa fedheha lakini uaminifu huzaa heshima.”Kileo akajiona aibu na kuapa kubadilika.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872



Post a Comment