Emakulata Msafiri
Twiga mrefu sana aliyekuwa na shingo ndefu kuliko wanyama wote.
Twiga alikuwa mpole, mkarimu, na alipenda kula majani ya juu juu ya miti. Lakini mara nyingi wanyama wengine walimcheka wakisema:
“Twiga wewe uko mbali sana juu, huwezi kucheza nasi!”
“Shingo yako ndefu inachekesha!”
Twiga alihisi huzuni, lakini hakuwajibu kwa hasira. Aliendelea kuwa mwema.
Lakini Twiga kwa sababu ya shingo yake ndefu aliweza kuona mbali sana. Akaona kijito kidogo cha maji kwa mbali, nyuma ya kilima kirefu.
Akarudi haraka na kuwaambia wanyama wote:
“Nimeona maji! Njoo twende wote tukunywe!”
Wanyama walishangaa sana na wakamshukuru Twiga.
Tangu siku hiyo, hawakumcheka tena, bali walimheshimu kama rafiki wa kweli.
Emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872
Post a Comment