TUWE WAAMINIFU KWA AHADI ZETU

 

Emakulata Msafiri

Siku moja fisi na sungura walikutana msituni. Fisi alikuwa na njaa sana lakini hakuwa na chakula. Sungura alikuwa na mahindi mengi aliyoyavuna kutoka shambani kwake.

Fisi akamwambia sungura, "Rafiki yangu nomba unipe mahindi yako yote. Nitakulipa baadaye."

Sungura akamjibu "Sawa nitakupa lakini uniahidi utanirudishia siku ya Jumapili."

Fisi akaahidi kwa moyo wake wote. Akachukua mahindi yote na kuondoka.

Siku ya Jumapili ilipofika fisi hakutokea. Sungura alingoja na kungoja lakini fisi hakurudi. Baada ya wiki moja sungura aliamua kumtafuta fisi.

Alipomkuta fisi alimcheka na kusema "Hakuna mahindi kwangu! Nenda zako!"

Sungura alihuzunika sana. Aliamua kamwe asimwamini tena fisi.

Msimu mwingine wa mavuno ulipofika fisi alipomwendea tena sungura kuomba chakula sungura alikataa. Akasema. "Ulivyofanya mwaka jana sitasahau. Mtu mwaminifu huaminika kila wakati."



emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments