Emakulata Msafiri
Karem alikuwa mtoto mdogo aliyeishi mjini na babu na bibi yake. Alikuwa anaogopa mambo mengi giza la usiku, kelele za magari barabarani hata paka wanaopita mitaani. Kila mara akiona kitu kisicho cha kawaidabalikimbilia kujificha nyuma ya bibi yake.
Siku moja usiku umeme ulikatika mjini. Giza lilitanda kila mahali. Karem akalia kwa sauti kubwa na kumkumbatia bibi yake. Babu yake akamwambia,
"Karem uoga si adui bali ni rafiki anayetuonya. Lakini tukiuacha ututawale hautaturuhusu kukua"
Siku iliyofuata Karem alitoka dukani na bibi yake. Wakati wanarudi paka mweusi akaruka ghafla mbele yao. Karem akataka kukimbia lakini akakumbuka maneno ya babu. Akasimama akapumua akaona paka yule hakuwa na madhara. Kwa utulivu akatembea karibu na bibi yake na wakaendelea na safari yao.
Bibi na babu walitabasamu wakamwambia "Umeanza kujua nidhamu ya uoga. Huo ndiyo mwanzo wa kuwa jasiri."
Tangu siku hiyo Karem alijifunza kwamba nidhamu ya uoga si kuishi bila kuogopa bali ni kujua jinsi ya kuukabili na kuutawala.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872
Post a Comment