SI KILA UKIPENDACHO HUBAKI MILELE

 

Emakulata Msafiri

Lina anapenda maua aliamua kupanda kwenye dirisha lake linaning’inia chungu kidogo cha udongo chenye ua moja jekundu. Kila asubuhi lina hufungua paziia huku akitatabasamu na kuzungumza na ua lake.

“Siku njema rafiki yangu " anasema kila siku.

Lakini leo Leo ua limelala. Majani yake yamepinda rangi yake imepotea. Lina anatulia kimya. Maji aliyompa jana hayajasaidia Ua lake limekauka.

Analiangalia kwa muda mrefu. Moyo wake unasononeka.

Mama yake anakuja na kusema “Lina si kila kilichopendwa hubaki milele. Wengine huondoka wengine huja.”

Lina anatoka nje anazunguka bustani. Kando ya uzio anagundua chipukizi dogo likichomoza ardhini jani jekundu changa kama tumaini jipya.

Anainama anachimba kwa upole na kulihamishia kwenye chungu alichoweka ua lake la zamani.

“Sijakusahau " ananong’ona kwa ua lililonyauka. “Lakini nitajifunza kupenda upya.”

Lina anafunga pazia lakini moyo wake uko wazi.


emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments