Emakulata Msafiri
Katika msitu mkubwa wa kijani aliishi nyati mwenye nguvu aliyeitwa Bwana Nyati. Alikuwa mkubwa, mwenye pembe nene na mwili mzito. Wanyama wengine walimwogopa kwa sababu ya mwonekano wake.
Bwana Nyati alikuwa mkarimu na mtulivu. Alipenda kusaidia wanyama wengine na hakuwa na kiburi hata kidogo.
Siku moja, chui mwenye njaa aliingia msituni. Alikuwa akiwinda wanyama wadogo. Kila mnyama alikimbia kwa hofu. Sungura,paka mwitu, na hata swala mdogo walijificha.
Bwana Nyati alipoona hali hiyo, aliuliza:“Kwa nini mnajificha?”Sungura akasema kwa sauti ya woga:
“Chui yuko karibu! Anatufuatilia!”Bwana Nyati hakukimbia Badala yake alisimama katikati ya msitu akatandika miguu yake chini kwa nguvu na kusubiri chui ajitokeze.
Chui alipotokea alimkuta Bwana Nyati akiwa imara. Alijaribu kumtisha, lakini Bwana Nyati akasema kwa sauti nzito:
“Hawa ni ndugu zangu. Ukitaka chakula, nenda mbali. Hapa hakuna anayeliwa!”
Chui aliona hofu kwenye macho ya Bwana Nyati. Hakupigana akaamua kugeuka na kuondoka zake msituni.
Wanyama wote wakamtazama Bwana Nyati kwa mshangao na furaha. Tangu siku hiyo, wakaanza kumuita:
“Shujaa wa Msituni!”
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872



Post a Comment