NGOMA YA MWANGAZA WA MWEZI

Emakulata Msafiri

Katika dunia iliyojificha chini ya ardhi ya kawaida kulikuwepo na mji wa ajabu uitwao Lumarea ambako viumbe waliitwa Waangavu waliishi. Hawa viumbe walikuwa na miili ya kung’aa kama mwezi walizungumza kwa midundo ya ngoma na walikuwa hawajawahi kuonekana na mwanadamu yeyote.

Kila mwaka wakati mwezi ukiwa mpevu zaidi usiku wa 13 wa mwezi wa saba Lumarea ulifanya sherehe takatifu iitwayo Ngoma ya Mwangaza. Ilikuwa ni sherehe ya kumwomba mwezi uendelee kuwapa nuru na maisha.

Mwaka huo kitu cha ajabu kilitokea. Amani msichana mdogo kutoka juu ya dunia ya wanadamu alianguka kwenye pango lililokuwa karibu na kijiji chao. Bila kujua akaingia kwenye lango la siri na kujikuta katikati ya mji wa Lumarea siku moja kabla ya Ngoma ya Mwangaza.

Waangavu walishangaa kumuona lakini hawakukasirika. Badala yake wakamuona kama alama ya mabadiliko. Walimfundisha kucheza ngoma yao wakitumia midundo ya moyo wake kama ala mpya. Usiku ulipowadia Amani akacheza pamoja nao na kwa mara ya kwanza mwanga wa mwezi ulishuka kama mvua nyepesi ya dhahabu.

Kwa kugusa ardhi ya Lumarea mvua hiyo iliwapa Waangavu uwezo mpya waliona ndoto za wanadamu na wanadamu waliota kuhusu mahali pa ajabu penye amani.

Amani alirudi juu duniani siku iliyofuata lakini kila usiku wa mwezi mpevu aliweza kusikia midundo ile ile ishara kwamba ulimwengu ule haukuwa ndoto tu bali ni sehemu ya moyo wake sasa.


emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments