MJI WA WANYAMA WENYE UMOJA

Emakulata Msafiri

Siku moja ukame mkali uligonga msitu. Maji yalipungua na chakula kilianza kuisha. Wanyama wengine walianza kuwa na hofu wengine wakaanza kugombania maji yaliyobaki.

Tembo aliyekuwa mzee mwenye busara alisema “Tukiendelea kugombana sote tutateseka. Hebu tushirikiane kutafuta suluhisho.”

Wanyama wakakubaliana kukutana kila asubuhi kupanga kazi. Simba akalinda usalama nyani akapanda juu ya miti kutafuta vyanzo vya maji ndege wakaruka angani kutafuta maeneo ya kijani na pundamilia na wengine walichimba mashimo kutafuta maji ardhini.


Baada ya siku kadhaa za ushirikiano ndege waliona kijito kidogo mbali msituni. Wanyama wote wakaelekezwa huko na kwa msaada wa tembo walichimba vizuri hadi wakapata kisima cha maji safi.

Mji wa wanyama ukarejea kuwa wa furaha. Wanyama walijifunza kuwa mshikamano na upendo ni muhimu hasa wakati wa matatizo.


emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments