Emakulata Msafiri
Kulikuwa na mji wa ndege. Ndege wa kila aina waliishi humo kwa amani: kunguru, njiwa, tai, kware, na hata kasuku.
Siku moja kulizuka ugomvi kati ya tai na kunguru. Tai alisema:
"Mimi ndiye bora kuliko wote kwa sababu naruka juu sana."Kunguru naye akasema:
"Bora wa kweli ni yule anayeishi karibu na watu siyo anayejificha juu mawinguni!"
Ndege wengine walianza kuchukua upande – baadhi walikuwa upande wa tai wengine upande wa kunguru. Hali ya mji ikawa mbaya sana. Hakukuwa na amani tena.
Kasuku aliyekuwa mzee wa mji aliamua kuwaita ndege wote kwenye mkutano.
Akawaambia: "Sisi sote ni tofauti, lakini kila mmoja ana umuhimu wake. Bila kunguru nani ataonya kuhusu hatari? Bila tai nani atatuonyesha njia kutoka juu? Hatuwezi kuishi kwa chuki."
Ndege wote walitulia na wakaanza kuelewana. Wakakubaliana kila mmoja awe na jukumu lake, na wakarejesha amani mji mzima.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872
Post a Comment