MCHEZO WA RIADHA KWA WATOTO

 

Emakulata Msafiri

Riadha ni mchezo unaohusisha kukimbia. Watoto wanaposhiriki katika riadha miili yao huwa na afya njema na nguvu.

Kuna aina nyingi za riadha kama vile mbio fupi, mbio ndefu, kuruka juu na kuruka mbali. Michezo hii huwafurahisha watoto na kuwajengea mazoea ya kufanya mazoezi mara kwa mara.

Riadha huwasaidia watoto kuwa na afya nzuri kuwa na marafiki na kuwa jasiri. Pia huwafundisha kushindana kwa heshima na kuvumilia wanapopoteza.

Mchezo wa riadha ni muhimu sana kwa watoto. Wazazi na walimu wanapaswa kuwahamasisha watoto kushiriki ili wawe na afya bora na furaha na pia itasaidia kuondokana na magonjwa nyemelezi.

Riadha ni miongoni mwa michezo ya msingi inayowafaa sana watoto kwa sababu huimarisha afya, hujenga misuli na kuwafundisha nidhamu. Watoto wanaposhiriki katika mchezo wa riadha hujifunza kushindana kwa heshima, kushirikiana na kujifunza uvumilivu.



emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments