Emakulata Msafiri
Lovely anashika karata zake kwa ustadi. Kwenye meza wachezaji wanne wamekaa kimya. Kila mmoja anasubiri zamu yake kwa tahadhari. Mchezo umefika hatua ya mwisho na karata zimebaki chache mezani.
“Lovely sasa onesha maajabu yako” anasema Rama huku akitabasamu.
Lovely haongei. Anaangalia karata yake ya mwisho joker. Anaidondosha mezani kwa ustadi. Wachezaji wote wanapigwa na butwaa.
“Umeshinda tena?” anasema Asha akiguna kwa mshangao.
Lovely anatabasamu kwa upole. “Mchezo ni akili si nguvu,” anajibu kwa sauti ya chini.
Wote wanapiga makofi. Furaha vicheko na vigelegele vinajaa hewani. Lovely anainuka anawashika mikono wachezaji wote.
“Leo ni zamu yangu lakini mchezo unaendelea kesho "anasema.
Karata zinakusanywa meza inafutwa na wachezaji wanapanga raundi mpya huku wakicheka na kubembelezana.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872
Post a Comment