Emakulata Msafiri
Katika jiji kubwa la Dar es Salaam palikuwa na jengo refu sana lililojulikana kama Mlimani. Likiwa na ghorofa 20 lilitumika kama ofisi, hoteli na pia kulikuwa na baadhi ya watu waliokodisha vyumba vya kuishi. Lakini kuna jambo moja la kushangaza hakuna ghorofa ya 13 kwenye paneli ya lifti. Baada ya ghorofa ya 12 lifti inaruka moja kwa moja hadi ya 14.
Watu walidhani ni imani za wazungu tu kwamba 13 ni namba ya balaa. Lakini wafanyakazi wa usafi walijua ukweli tofauti.
Fatuma alikuwa mfanyakazi mpya wa hoteli kwenye jengo hilo. Usiku mmoja alipangiwa zamu ya kusafisha ghorofa 10 hadi ya 15.Saa nane usiku akiwa peke yake aiingia kwenye lifti. Alipofika ghorofa ya 11 lifti ilisimama ghafla taa zikaangaza na kuzimika kwa sekunde kadhaa. Aliposhtuka aliona namba mpya kwenye paneli: 13 haikuwa hapo awali.
Kwa hamu ya kufuatilia alibonyeza. Mlango ulifunguka taratibu… mbele yake kukawa na korido ndefu sana yenye taa za kijani hafifu. Ukuta uliochakaa sakafu iliyokuwa na alama za damu zilizokauka na sauti ya kelele ndogo ya muziki wa piano ilisikika kutoka mbali.
Alitembea polepole moyo wake ukidunda kwa kasi. Mlangoni mwisho wa korido kulikuwa na kibao kilichoandikwa kwa herufi ndogo:
“Waliopotea walijibu mlio.”
Akiwa anatazama mlango ulifunguka polepole bila kuguswa. Nje hakukuwa na mtu. Lakini alipogeuka kuondoka aliona kivuli chake kikisimama mbele yake lakini kivuli hicho kilikuwa kinatabasamu na hakikufuata mwili wake.
Ghafla milango yote ikafungwa. Taa zikazimika simu yake haikupata mtandao. Fatuma alipotea.
Asubuhi yake walinzi walikuta lifti imesimama kati ya ghorofa ya 12 na 14. Ndani kulikuwa tupu ila kwenye kuta kulikuwa na alama za viganja vya damu na maneno yaliyokuwa yamechorwa kwa kucha:
“Ghorofa ya 13 haijawahi kufutwa Inawasubiri wapya.”
Mpaka leo kila mwaka tarehe aliyopotea Fatuma namba ya 13 huonekana tena kwenye paneli ya lifti kwa sekunde chache tu na mara nyingine mtu huingia humo… na hapatikani tena.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872


Post a Comment